8 PRINCIPLES
KEEP FAITH

What do you hold on to when you have done your part, but nothing seems to be changing?
Waiting can make you question everything. You send the application and hear nothing. You work on a dream while the bills keep coming. You pray, try again and still wonder how much longer you can keep going.
When disappointment takes over, you can begin to treat a difficult season as the whole story. Keeping faith leaves room for another possibility. It can help you face today with hope and take a useful step even while the outcome is uncertain.
Keeping faith means staying rooted in what gives your life meaning while you face what is real. For you, that may begin with trusting God, making time for prayer and leaning on a community that cares. You can have questions, feel afraid and still have faith.
Here are three ways to practice it:
1. Be honest about where you are.
Name what is worrying you. Write it down, bring it into prayer or share it with someone you trust. You do not have to pretend you are fine to find the strength to continue.
2. Remember what has helped you before.
Recall one difficult moment you got through. What supported you? A person, a prayer, a lesson or a small daily habit? Choose one source of support you can return to today.
3. Pair your hope with one action.
Send the application, ask for advice or finish the task in front of you. Give your attention to what you can influence, and allow yourself to seek help with what you cannot carry alone.
Faith does not promise that every plan will work out the way you want. Sometimes moving forward means grieving a loss, changing direction or beginning again. A different path can still lead to a meaningful life.
Start today, right where uncertainty meets your next decision.
Write down one concern. Beneath it, write one small action within your control. Take that step, or contact someone who can help you take it.
You do not need to see the whole road to take the next step with hope.
NEXT PRINCIPLEBE DISCIPLINEDUnashikilia nini unapokuwa umefanya sehemu yako, lakini hakuna kinachoonekana kubadilika?
Kusubiri kunaweza kukufanya uanze kuhoji kila kitu. Unatuma maombi bila kupata jibu. Unaifanyia kazi ndoto yako huku bili zikiendelea kuja. Unaomba, unajaribu tena na bado unajiuliza utaweza kuendelea kwa muda gani.
Kukatishwa tamaa kukitawala, unaweza kukiona kipindi kigumu kama maisha yako yote. Kudumisha imani kunakupa nafasi ya kuona uwezekano mwingine. Kunaweza kukusaidia kuikabili leo kwa matumaini na kuchukua hatua yenye manufaa hata kama hujui matokeo yatakuwaje.
Kudumisha imani ni kuendelea kushikilia kinachoyapa maisha yako maana huku ukikabiliana na hali halisi. Kwako, inaweza kuanza kwa kumtumaini Mungu, kutenga muda wa maombi na kutegemea watu wanaokujali. Unaweza kuwa na maswali, kuhisi hofu na bado kuwa na imani.
Hizi ni njia tatu za kuanza:
1. Kubali kwa uaminifu hali uliyonayo.
Taja kinachokutia wasiwasi. Kiandike, kipeleke kwenye maombi au mshirikishe mtu unayemwamini. Huhitaji kujifanya uko sawa ili kupata nguvu ya kuendelea.
2. Kumbuka kilichokusaidia hapo awali.
Kumbuka wakati mmoja mgumu uliouvuka. Nini kilikusaidia? Mtu, maombi, somo au tabia ndogo ya kila siku? Chagua chanzo kimoja cha msaada unachoweza kukirudia leo.
3. Unganisha matumaini na hatua moja.
Tuma maombi, omba ushauri au kamilisha kazi iliyo mbele yako. Elekeza umakini kwenye unachoweza kuathiri, na ukubali kutafuta msaada kwa yale usiyoweza kubeba peke yako.
Imani haiahidi kwamba kila mpango utafanikiwa kama unavyotaka. Wakati mwingine kuendelea mbele kunamaanisha kuomboleza ulichopoteza, kubadili mwelekeo au kuanza tena. Njia tofauti bado inaweza kukupeleka kwenye maisha yenye maana.
Anza leo, hapo ulipo, unapokabili uamuzi unaofuata bila kuwa na majibu yote.
Andika jambo moja linalokutia wasiwasi. Chini yake, andika hatua moja ndogo iliyo ndani ya uwezo wako. Chukua hatua hiyo au wasiliana na mtu anayeweza kukusaidia kuichukua.
Huhitaji kuona barabara yote ili kuchukua hatua inayofuata kwa matumaini.
KANUNI INAYOFUATABE DISCIPLINED